John 17:2-6

2

aKwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa.

3

bNao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Isa Al-Masihi uliyemtuma.

4

cNimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye.

5

dHivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwepo.

Isa Awaombea Wanafunzi Wake

6 e“Nimelidhihirisha jina lako kwa wale ulionipa kutoka ulimwengu. Walikuwa wako, nawe ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako.
Copyright information for SwhKC